Saturday, September 29, 2007

SIMBA NA YANGA SI TIMU KUBWA BALI TIMU KONGWE!

Makala ya aliyewahi kuwa kocha wa Simba na Y anga kwa nyakati tofauti Siller Said Mziray leo katika gazeti la Mwanaspoti yamenifurshisha sana, ameandika kuwa timu za Simba na Yanga si timu kubwa katika soka la Bongo bali ni timu kongwe tu nchini ukilinganisha na timu zingine zinazoshiriki ligi ya VodaCom.Kwa kweli ameeleza ukweli mtupu.Ni kama nilivyosema katika makala yangu mojawapo kuwa zile zama za kufikiria kuw Simba na Yanga kuwa wao ndo kila mwaka watakuwa wafalme wa soka katika nchi hii kwa kweli zimepitwa na wakati.Hapa lazima ieleweke kuwa hizi timu hazitofautiani sana kwa kiwango cha soka bali zinazidiana uwezo wa kimaslahi kutokana na kuwa timu hizi ni kongwe na zina wapenzi wengi,wafadhiri wengi na vitu kama hivyo lakini kuhusu soka au kiwango cha kucheza wala havipishani sana na ti.mu zingine zinazoshiriki ligi ya VidaCom.
Hongera Mziray umeongea ukweli mtupu hata kama wadau wengine hawatakubali.Lakini ni sawa kabisa kuwa Simba na Yanga ni wakongwe tu wa soka la Bongo na kamwe wsijindanganye kuwa ni timu kubwa.Timu kubwa hazina wala uwanja wa kufanyia mazoezi achilia mbali mechi,timu kubwa hazina hata utaratibu unaoeleweka kuhusu wachezaji wake na timu kwa ujumla,timu kubwa zinakimbiwa na makocha kila kukicha na mbaya zaidi wanakimbiwa hata na makocha wazalendo je kunani pale Simba na Yanga?Ni ubabaishaji na uswahili mkubwa ndo unatawala pale.Wale wote wanaohusika na majukumu ya timu mbili hizi lazima wasome alama za nyakati na wakubali mabadiliko haraka sana.Simba na Yanga sisi ni wapenzi,wanazi wenu wakubwa kubalini mabadiko hizi ni zama zingine vinginevyo mtakuwa mnarudi nyuma daima badala ya kuenda mbele.Jiulizeni timu kama ElMerreikh miaka michache nyuma ilikuwa timu ya kwaida lakini leo hii angalia jinsi ilivyo angalia jinsi inavyomlipa kocha wake angalia inavyochanja mbuga katika soka la Afrika ina wachezaji wa kulipwa mpaka kutokaBrazil na imepiga hatua sana jamani.SIMBA ,YANGA TUACHE UBABAISHAJI KATIKA SOKA TUKUBALI MABADILIKO ILI HIZI TIMU ZIWE ZENYE KUOGOPEWA NA KUHESHIMIWA HAPA AFRKA HIZI NI TIMU KUBWA JAMANI ACHENI KUZIDHARIRISHA NINYI WADAU NA ACHENI KUWA HAPO KWA MASIRAHI YENU BINAFSI MUWE HAPO KWA FAIDA NA MAENDELEO YA MPIRA WA NCHI HII JAMANI HAKUNA LISILOWEZEKANA KWANI WAO WAWEZE WANA NINI NA SISI TUSHINDWE TUNA NINI.WAKATI NI HUU!TWENDE TUJIANDIKISHE SASA!

MASHAMBA YA MIWA YA MTIBWA!

Mtibwa Sukari ni eneo linalotoa picha ya kuvutia sana,upande wa mashariki wa eneo hilo limezungukwa na mashamba takribani ekari elfu nne za miwa,kota za wafanyakazi,kiwanda chenyewe cha sukari,miji midogo ya Mabau,Kidudwe,Mji unaokuja kwa kasi wa Madizini,hospitali ya Bwagala,mji wa Turiani mji wa Lusanga pamoja na shule yake maarufu ya sekondari ya Lusanga,chuo cha ualimu Muhonda na maeneo mengine mengi mazuri na ya kupendeza kama Kanga,Dihinda,Kwewmtonga,Mwenvuge,Divumbasa,Mlaguzi Chazi,Kigugu,Mbogo[Mtego wa Simba] Mkindo,Diongoya,Sungaji na maeneo mengi ya kuvutia bial kusahau milima tulivu na inayovutia milima ya Nguu.Kwa kweli maeneo haya yanatoa picha ya kupendeza sana.
Huko kuna timu ya mpira wa miguu ya Mtibwa Sukari ni eneo zuri na tulivu sana lakini kama unafika kwa mara ya kwanzxa unaweza ukataka kurudi leoleo!waja leo warudi leo lakini ukikaa kw siku kadhaa hutatamani kuondoka!Ardhi ina rutuba hali ya hewa nzuri maeneo yanavutia jinsi kulivyo ni kama tukichukua mtaa mmoja wa Dar acha tuseme kama Siza vile ndivyo kunavyofanana mahala pale.Nimewahi kuishi kule hususan maeneo ya Chazi Hospitali na nimekuwa na ndoto ya kuishi maeneo yale kwa maana yananivutia sana.Hata Salome Ihembe a.ka. Salome Leng'alwa analitambua hilo.Tukijaaliwa katika siku za usoni ninapenda sana kuhamishia makazi yangu huko,Turiani,Chazi,Mtibwa na maeneo ya jirani kwa kweli kwangu mimi yanatoa picha ya kupendeza sana.Salome upo!Mtibwa Sukari na hatima ya soka la Tanzania!Wasalimie Manungu!

MSAFIRI KAFIRI!

Jumamosi leo wiki endi mapumziko kwa wengi wetu baada ya wiki nzima ya kuchakarika na kazi zinazotuhusu,watu ni wengi Kariakoo,Posta,mitaa ya Kisutu na kila kona ya jiji.Kila mtu anajaribu kupata kile kilichomtoa nyumbani mchana huu.Madukani ni mshikemshike sokoni Kariakoo ndo usiseme,mtaa wa Msimbazi ni balaa tupu kuna mabasi mawili yamekodishwa na wapenzi wa Simba wanaojiita matawi ya mpira pesa wanajinadi kuwaeleza abiria kuwa usafiri upo wa kwenda Mji kasoro bahari kushuhudia pambano la mpira kati ya Simba na timu ya Pan Afrian[Twiga] ya Kinondoni.
Napita katika maduka ya TV nataka kununua TV maana ligi ya Uingereza siku hizi tunaifaidi kupitia TV ya Taifa shukurani kwa Tido Mhando kuwezesha sisi walala hoi kuona mpira wa kweli.Wauzaji wote hakuna anayesema ukweli kila mtu anavutia kwake unajua kilichotokea nimeamua kuachana na manunuzi ya TV nitanunua ya mtumba lakini sizipendi kwa kuwa zinachangia kuchafua mazingira ya hapa Bongo maana kwa nini zije huku wakati huko kwao zimeishatumika kwa nini watuletee siosi?Basi sitanunua kabisa!Ukipita madukani wote wanauza wanatumia lugha nzuri sdana na wana nidhasmu ya hali ya juu huwezi amini.Kweli sasa hivi Bongo biashara ni biashara huria!
Nimechoka kuzunguka madukani nipo Rik Pub nyuma ya jengo la Washirika nimeagiza msosi unapigwa wiombo wa Msafiri Kafiri navutiwa nao maana mimi ni penzi wa Msondo si unakumbuka jana nimeelezea kuhusu wimbo wa Msondo wa Nidhamu ya Kazi?
Hapa unapigwa Msafiri Kafiri kwa kweli nimechanganyikiwa mimi ni Mnazi mkubwa sana wa Msondo:
Msafiri kafiri mwenda pole hajikwai akijikwaa haumii kuumia kwake kidogo tuu
Mimi msafiri kafiri nakuja nawapisha wale waendao na warudio kwa haraka mimi naja taratibu!Msondo NGOMA YA wATANZANIA!WANACHEZEA UMEME HAO WATANASA SASA HIVI!

Friday, September 28, 2007

NIDHAMU YA KAZI.

Msondo ngoma baba ya muziki wana magoma kitakita wale jamaa kiboko kwa tunzi zao mbalimbali.Nyimbo kama "NIDHAMU YA KAZI" kwa kweli ni moja ya nyimbo zenye ujumbe mzuri sana kwa jamii.Maana kazi ndiyo msingi wa maendeleo,kama alivyowahi kusema Baba wa Taifa "Kazi ndiyo msingi wa maendeleo,nchi masikini haiwezi kuendelea kama inategemea fedha kuwa ndiyo msingi wa maendeleo,nchi masikini haiwezi kuendelea kama inategemea misaada kutoka nchi za nje"Maneno haya aliyasema wakati anafungua uwanja wa Mapinduzi[uwanja wa Sokoine]Mbeya.
Nidhamu ya kazi ni msingi wa mafanikio mema kazini
Viongozi na wafanyakazi lazima sote tuwe na nidhamu
Migogoro na migongano ya kazini ni ukosefu wa nidhamu
Viongozi pia wajibu wenu mkubwa ni kulinda heshima
N kudumisha nidhamu ya kazi
Haya yote ni rahisi kuapatikana iwapo tutatia maanani suala la nidhamu!

Thursday, September 27, 2007

SHULE YA MSINGI KIGUGU-2

Habari hii nimeitoa kwa ufupi lakini bado ninaitafutia muda ili niiandike kwa kirefu kwani ni habari ndefu kidogo ambayo ina mambo mengi sana yaliyotukia enzi hizo tukiwa shule ya msingi Kigugu kule Chazi Turiani Morogoro Vijijini enzi hizo siku hizi ni wilaya ya Mvomero.
Nitakuja na majina ya ajabu ya wanafunzi tuliosoma nao kama Veronika Mezanyoka,Augustino Mkeka,Rose Mdudu Chanzala ThomasSamboa Akisa,na jamaa aliyeibia wakati wa mtihani akaandika mpaka jina la yule aliyekuwa akiibia mtihani wake!

MADEREVA,MAKONDA VS WANAFUNZI!

KITUO CHA KARUME:
DALADALA:TABATA-SEGEREA:
MUDA:JIONI:
Wakazi wa Segerea wengi wetu lazima tupandie hapo Karume tukageuze na basi mpaka mnazi Mmoja mana usafiri wa Segerea ni taabu kwelikweli.Konda kasimama mlangoni tunaingia bila wasiwasi maana si twaenda kugeuza nalo,tunalipa mara mbili "Kongo Mnazi ikirudi Segerea!"Konda kamuona mwanafunzi hana makuu mwanafunzi yule mpole konda anamzuia mlangoni dogo anafanikiwa kuingia anakaambele kwa dereva mahala pasipo na kiti,nmi nipo mbele dereva "Mangi" anaanza kumfokea kwa nini unafanya vurugu mlangoni ukiumia nani atakulipa?Anamtukana dogo kakaa kimya tu kachoka na anaonyesha woga.Naingilia kwani kafanyaje?Anajibu hujamuona kafanya vurugu mlangoni namuuliza vurugu gani maana konda kamzuia sasa angeingiaje?Anajibu wewe unatetea ujinga wewe mpumbavu namjibu wewe ndo mpumbavu maana mtoto hajafanya vurugu unasema kafanya vurugu.Tunajibizana mpaka mnazi.Pale watu kibao sasa ndo wanafanya vurugu za kweli na wanaweza kuumia kwa kugombania basi namtazama dereva kwa chati halafu nacheka sana sana mpaka watu wananishangaa nafikiri jibu amelipata kwa nini ninacheka ni kuwa je wale watu wote wakiumia kwa kugombania basi atawalipa?Maana wamefanya vurugu n yule dogo pale Karume hakufanya vurugu kaambiwa kuwa anafanya vurugu akiumia nani atamlipa?
Wanafunzi wanapata taabu sana katika jiji hili hasa nyakati zza asubuhi na jioni,wanakatazwa hata kukaa hata kama basi halijajaa.Ugomvi wa kijana yule na koda na dereva kisa ni 50/= anayolipa ndiyo inamfanya asithaminiwe utu wake.Lakini si yeye anayepanga bei hiyo yeye anaathiriwa na mfumo tu jamani.
Na nimechunguza sana madereva na makonda vijana ndiyo wanawanyanyasa vijana wenzao wadogo zao.Lakini fanya utafiti utagundua kuwa makonda na madereva watu wazima wenye familia kamwe hawawanyanyasi wanafunzi na iwapo imeshindikana kuwachukua watawaeleza kistaarabu,binafsi nimewahi kumshuhudia konda wa makamo akiwakataa watu wazima na kuwachukua wanafunzi watoto wadogo nyakati za jioni ili wawahi nyumbani!Iinapaswa wengine waige mfano huo japo kwa kutoa lugha ya kistaarabu jamani.

TIMU NDOGO ENDELEZENI VIPIGO ALUTA CONTINUA!

Hakuna aliyetarajia kuwa Wakongwe wa soka hapa nchini?Au wavurugaji wa soka hapa nchini?Kuwa wataangukia pua mwishoni mwa wiki iliyopita katika safari ndefu ya kusaka bingwa wa Tanzania bara wa soka msimu wa 2008/2009.Simba na Yanga wameonja makali ya kufungwa katika mechi zao za mwanzo kabisa msimu huu.Binafsi nimefarijika sana na vipigo hivyo kwa hawa wavurugaji wa soka la hapa Bongo.Hii ni changamoto kwa viongozi na wapenzi wa timu kubwa hizi mbili ambao wamejikita katika mawazo ya kuwa wao ndo kila kitu katika soka la Bongo na kuwa bila wao hakuna kitu kiitwacho soka kinaweza kufanyika hapa Bongo.

Wadau wa timu kubwa hizi mbili kwa kweli wanashindwa kusoma alama za nyakati kuwa kwa zama hizi ni kuwa soka linapita katika mabadiliko makubwa sana hasa baada ya kuwa timu yetu ya Taifa imeboreshwa kwa kiwango cha kuridhisha na kuwa kamwe wasitegemee timu kama Ashanti kuwa zama hizi inaweza kucheza bila ya malengo kamwe kamwe maana kila ndoto ya mchezaji wa nchi hii katika timu hizi ni kuwa na mafanikio makubwa katika soka hili la kisasa ambalo kwao linalipa siku hizi.

Wachezaji wa timu hizi ndogo siyo kuwa hawana akili wanajua kuwa hizi ndiyo nafasi zao adimu na pekee kwa wao kuonekana ili kuchaguliwa timu ya taifa na hatimaye kuweza kuonekana na kupata timu nje ya nchi ili kukuza vipaji vyao na kuendelea kimaisha.

Binafsi ni mnazi mkubwa wa Simba lakini napenda kusema hadharani kuwa ushabiki wangu ni tofauti kidogo na wanazi wengine wa timu kubwa hizi.Mimi naishabikia Simba iwapo inaonyesha kiwango kizuri,na haibebwi na marefa au watu fulanifulani wenye marengo yao binafsi. Lakini kama naona kuwA ushindi wake una mizengwe na ni wakutiliwa mashaka kamwe huwa siwi upande wao!Pia kama timu ya Yanga inacheza vizuri mechi za nje yaani za kimataifa basi huwa ni mmoja wa mashabiki wanaojumuika na wanayanga kuipa sapoti ya kuishangilia.

Huwa napenda sana timu kubwa hizi zinapokutana zenyewe au zichezapo na timu pinzani basi zishinde kwa uwezo wa timu na si kwa uwezo wa watu fulani wachache,hapa ndiyo maana nafika mahala nasema kuwa timu hizi ni wavurugaji wakubwa wa soka la bongo.

Lazima Simba na Yanga watambue kuwa Kukua kwa viwango vya mpira katika timu hizi si kwa mmoja kumfunga mwenzie bali ni kuwa na mikakati madhubuti ya kuhakikisha kuwa zinakuwa moja ya vilabu vikubwa kabisa katika ukanda wa soka wa Afrika na wakidhamiria wanaweza.

Wasipende kuwa na wachezaji wa magazetini au kuwa na wachezaji wa kusifiwa na wapenzi wao mara baada ya usajili na kuonekana mazoezini na kusifiwa kuwa safari hii timu yetu kiboko makombe yote yatakuwa yetu huu mwaka wa vikombe Msimbazi,huu mwaka wa vikombe Jangwani na vitu kama hivyo.Mpira siyo mdomoni mpira ni uwanjani na maandalizi ya muda mrefu na yenye marengo.Mpira tofauti na msanii wa Runinga kuwa anaweza akatunga kitu hapohapo na akapata mashabiki.Simba na Yanga imefika wakati sasa waelewe kuwa mpira siyo "Masanja Mkandamizaji",mpira siyo "Uswahili" mpira kazi kama kazi zingine.

Naelewa kuwa kufungwa huku na kutoka sare kutawafanya waanze kutafuta mbinu za ziada ndani na nje ya uwanja nasema hizo hazitawasidia maana watanzania sasa wamekuwa waelewa kwani watazigundua mbinu hizo hata kama watakuwa wanashinda kwa msaada wa watu fulanifylani lakini lazima watambue kuw mbinu hizo hazitawafikisha popote cha muhimu ni kuucheza mpira na kuacha usanii.Waache timu bora zishinde na wala siyo bora timu ishinde.

Ashanti,Coastal Union nawapongeza sana kwa kuvikandamiza vigogo mmenikumbusha enz ya Relinya Morogoro.Cha msingi msibweteke safari bado ni ndefu na hizi timu zina mbinu nyingi sana ya kuweza kukudhoofisheni.SIMAMENI IMARA PIGANIENI HAKI ZENU KWA KUCHEZA MPIRA NA KUWA MAKINI MUDA WOTE WA MCHEZO!KUMBUKENI KUWA SIMBA NA YANGA ZINA MBINU NYINGI SANA.MSIBWETEKE.MSIJE MKAWA KAMA WAPIGANAJI WA OMAR TUPAC SHAKUR MILITIA MOVEMENT WALIPOTEKA UBALOZI WA JAPAN KULE LIMA,PERU 1997 WAKAJISAHAU NA ULINZI WAKAANZA KUCHEZA SOKA KAZINI,UNAJUA KILICHOWAKUMBA?MAKOMANDOO WAKAWAVAMIA PASI NA HABARI NDO IKAWA IMETOKA HIYO!SIMBA NA YANGA NI MAKOMANDOO NA MAFIA WA SOKA LA KIBONGO MSILALE LETENI MAPINDUZI YA KWELI HATA WAKIPENDELEWA WATU WATAONA!ASHANTI,COASTAL NA TIMU ZOTE CHANGA ALUTA CONTINUA!JIKWASMUENI NINYI WENYEWE KUTOKA KATIKA MAKUCHA YA SIMBA NA YANGA NA HAKUNA MTU ATAKAYEWABEBA BALI NI NI NINYI WENYEWE!SIMAMENI IMARA HAKI ZENU ZITAPATIKANA KWA SOKA LENU LA KUVUTIA,WAKATI WA SOKA LA VURGU KWENU ULISHAPITWA NA WAKATI ONESHENI MNAWEZA WATU KIBAO WAPO NYUMA YENU!USHINDI NI DHAHIRI!ASANTENI.

Tuesday, September 25, 2007

SOPA LODGE,NGORONGORO KRETA! 2005-2006:

Sehemu ya kuvutia mojawapo ya yanayosemwa maajabu ya dunia.Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu ninaiona kretakwa mbali toka katika hii hoteli ya Sopa Lodge amabayo tumekuja kufanya majaribio kwa vitendo kwa muda wa miezi mitatu.
Watu wakarimu hapa na tumepokelewa vizuri sana jamaa kaja mpaka ndani ya gari kuja kutupokea na kutuonyesha wapi tutapumzika kwa usiku huo tuliofika.Baridi ni kali sana tumepewa blanketi mbilimbili lakini bado tunasikia baridi.
Kesho yake tunaonyeshwa kwa uongozi wa hoteli na kupangiwa majukumu ya kujifunza kwa muda huo wa miezi mitatu,kutoka Disemba mpaka Machi mwaka ujao.
Tunachapa kazi wanachuo tuliotoka mjini Arusha katika chuo cha mafunzo ya hoteli.Tunaanza kuzoeana na wafanyakazi,dada mmoja mweupe kwelikweli anatuzoea na kutupa majina ya utani "wanafunzi wangu".Dada huyu ananizoea sana mimi kuliko mwenzangu Tom aasema mimi mcheshi na ninatoka Dar na yeye anasifia Dar anadai huwa anakuja mara nyingi kwa jamaa yake.Baada ya siku kadhaa Mkuu wangu wa jiko hataki kuona huyu dada ananizoea anaanza kuwa makali kwangu na kufoka bila sababu baada ya kuchunguza kumbe ati alimfundisha mambo mengi ya upishi na inadaiwa ni bibi yake sasa Mpishi anawasiwasi naweza fanya mapinduzi baridi!Anakuwa mbogo ile mbaya.Naona naonewa naamua kuwaka siku moja usiku ile mbaya mpaka walinzi wa hoteli wanashangaa huyu Trainee haogopi anamwakia jamaa ile mbaya.Rafiki yangu Ray ananifuata asubuhi anasema safi sana usingeonyesha msimamo angekunyanyasa sasa atakuwa anakuogopa!
Huko ni hotelini.Njoo sasa kambini mahala tulalapo,madereva wa Tours wnanishangaa jamaa anamuuliza mwenyeji eti masai huyu jamaa naye ni Trainee?anaambiwa ndiyo anasema hapana sasa tunadanganyana sasa tumeanza kuletewa wapelelezi kambini!Unajua kisa cha jamaa kusema hivi?Kiumri kwa sisis tuliokuja kujifunza mimi ni mkubwa pamoja na mwenzangu Tom lakini waliobakia wote ni vijana waliomaliza shule ya sekondari mwaka jana au juzi sasa mimi jamaa wanashangaa nina kipara kikubwa sana hata mwanzoni askari mmoja wa TANAPA alifikiri nanyoa kama mtindo!Njaribu kuwaeleza kuwa ukubwa wa umri si kikwazo katika kusaka ujuzi.
Napata marafiki wengi sana wa Kimasai na watu wa sehemu mbalimbali wengine wananiita Babu,wengine wananiita Mourinhonmaana kwa mpira ndiyo usiseme naupenda na nimekuwa nikiwapa data hata za miaka ya nyuma sana.
Kombe la Mataifa ya Afrika linaanzaMisri Januari hiyo bado tupo mafunzoni napangiwa shift mbaya sana wakati musada wa mechi inaanza.Nampiga kamba kiongozi wangu inabidi nidanganye kuwa huwa napata "majani" kidogo sasa naomba nikapate ingawaje sijawahi kupata majani hata siku moja jamaa anasema wewe nenda usichelewe kurudi nakimbia kambini nacheki kama dakika 30 narudi tena.
Maisha yanenda napata marafiki wengi na kujifunza kazi nyingis sana.Lakini katika yote niliyoyaona Ngorongoro Nilishangazwa na kupendezwa sana na Kreta.Nilipofika chini kabisa kule kwa mara ya kwanza nilichanganyikiwa sikuyaamini macho yangu.Dr.Remi aliwahi kuimba kuwa tembea ujionee usingoje kuambiwa huwezi ukafananisha Morogoro na Dar es salaam ni kweli Ngorongoror ni mojawapo ya maajabu ya dunia!Kwa kweli kunapendeza sana!

Monday, September 24, 2007

SHULE YA MSINGI KIGUGU.

Shule ya msingi Kigugu ndiyo shule yangu ya kwanza kabisa 1976 mdogo kabisa miaka sita siku ya kwanza kwenda shule nililia sana naamshwa kwenda shule sitaki kisa mimi mdogo kwa nini niende shule?SHULE YETU!Unajua darasa lilipokuwa chini ya mwembe mwalimu wangu wa kwanza kunifundisha mwalimu Magdalena Ngwego tunaanza kwa kuandika chini au kuchora chini njaa inaniuma naamua kutoroka nakutana na akina mama wamepita maeneo ya shule naambiwa ahaa unatoroka shule tunaenda kukusemea kwa baba.Jamani tumetoka mbali lakini shule ni muhimu sana ila kufuatana na mazingira unayokuwa nayo wakati mwingine unaona kama ni jela ya sirisiri kama alivyowahi kuandika kwenye ukuta mwanafunzi mmoja kule Iyunga sekondari."Elimu ni ufunguo wa maisha"Nitaandika mengi sana kuhusu shule yangu ya kwanza ya msingi Kigugu Turiani,Morogoro.

NIMEKUWA MZEMBE,NILISAHAU NAMBA YANGU YA KIFICHO!

Unajua sijui nijiite mzembe au msahaulifu hata sijui nisemeje,kwa kweli nilisahau namba yangu ya kificho hata nashindwa sijui nisemeje,eti nimehangaika sana leo ndiyo nimebahatika kuipata.Kwa kifupi hii blog yangu niliifungua toka February 2004 hebu fikiria miaka karibu mitatu lakini nikawa nashindwa hata kuandika kitu cha kuipa jamii kwa kujifanya niko bize sijui bize gani?Bize nitakuwa mimi bwana bize wako kina Ndesanjo maana wao kila kukicha wanahangaika kila mahala kutuhabarisha na kutuelimisha.
Lakini baada ya kusoma tena na tena makala ya Ndesanjo yatokayo katika gazeti la Mwananchi kuwa kila mtu ni mwana habari haijalishi kuwa kasomea au la lakini pale alipo na akiona habari yoyote basi ni habari basi nikashawishika kuwa anagalau niwe ninajitahidi kuwapatia wanajamii habari mbalimbali zitukiazo katika maisha yetu ya kila siku.
Bwana Boaz A. Boaz Mwandishi wa zamani wa gazeti la shule Kantalamba 1991-1993 "Daily Vision" nashukuru kwa komenti yako na kuni unga mkono hasa kutokana na matokeo ya Taifa Stars na The Mambaz pia nilijaribu kumuuliza mchezaji mahili wa zamani wa Tanzania Sekilojo Jonson Mbwambo Chambua a.k.a. baba Lisa naye akasema kuwa matokeo yale aliyatarajia kwa maana kuwa wachezaji wa sasa wanapewa kila kitu lakini hawana mbinu afya maarifa nguvy na ari ya kutetea taifa lao.
Cha msingi kama nilivyoseni kuwa inabidi tugeuke nyuma kuangalia soka la watoto na vijana na kupata waalimu bora na wenye mbinu ya kuwafundisha hao vijana na ikiwezekana zianzishwe shule maalumu za soka kama kweli tunataka tufanikiwe na kamwe tusitake mafanikio ya njia za mkato hayo kamwe katika soka hayapo.Tutafanikiwa kama tutaanza sasa wala hatujachelewa!Asante

Tuesday, September 18, 2007

TUMEJIFUNZA NINI KIPIGO CHA MSUMBIJI?

Wengi walikuwa na matumaini makubwa sana kuliko uwezo wa timu yetu ya Taifa baada ya mchezo wa kule Burkina Faso na kabla ya mchezo na ndugu zetu wa damu Msumbiji.Wachache sana tulitegemea au kutarajia kuwa lolote linaweza kutokea katika mechi ile maana nao Msumbiji wana uzoefu na pia walikuwa wnajiandaa.
Katika mchezo wa mpira kuna vitu vingi sana hata bahati pia ipo.Inawezekana kabisa kuwa tulikuwa na bahati BurkinaFaso na inawezekana pia Msumbiji walikuwa na bahati hapa kwetu.Lakini kusema ule ukweli ni kuwa siku ya mechi na Msumbiji wale jamaa walituzidi sana na hii inawezekana ilichangiwa siyo tu kujiamini kwa wachezaji wetu bali pia hata sisi washngaliaji na tukasahau majukumu yetu ya kumuua Mamba.
Hatimaye baada ya mchezo timu bora ikashinda hilo halina ubishi.Lkini je tumejifunza nini wtanzania?
Tusiwe watu wa kukata tamaa mapema kiasi hicho!Timu yetu ndiyo kwanza inajengwa tutakuja kuyaona tu mafanikio na kamwe tusipende mafanikio ya mkato.Ipo siku penye nia pana njia tushikamane tuwe pamoja tuwe wamoja kwa kushirikiana tutakuja kuyaona matunda baadaye na iyo sasa wakati ni huu shime shime!Ushindi waja!