Thursday, November 29, 2007

WATANZANIA KUNDI LETU NDILO GUMU WALA SI RAHISI!

Kuna baadhi ya watu wameanza kuwadanganya watanzania nasi watanzania ni wepesi wa kuamini mambo ambayo kwa hakika huwa si ya kweli kabisa!Kumbuka jinsi watu walivyokuwa na matumaini ya kwenda Ghana kila mmoja alijua kuwa mwakani sote macho yetu kideoni tukiwashangilia Stars na Stars nao masikini wakaanza kuvimba vichwa wakati hata safari bado ilikuwa mbichi kabisa!Kumbuka jinsi walivyokuwa na nyodo wakati wanakwenda kucheza na Zambia kule mji unaotamani angalau kuwa na bahari japo kwa siku moja,Morogoro,washabiki waluguru wale wamefika Msamvu kuwalaki wachezaji wao lakini Stars wakawafungia vioo maana tayari wao wameishakuwa wafalme!
Ninachotaka kusema siyo kukatisha tamaa la hasha bali kuwaasa watanzania wenzangu kuwa kundi letu si rahi ni gumu sana na pengine ndilo kundi gumu kuliko makundi yote katika safari hii ya kuwania tiketi ya kucheza kombe la dunia.
Tukumbuke kuwa kwa soka la kisasa hakuna kitu kinachoitwa timu rahisi au kundi rahisi kama nilivyosema jana kuwa mpira ni mchezo wa maandalizi kama mitihani,mpira ni mchezo wa kujitoa,kujituma,kupambana na si kucheza soka ya midomoniambayo ndiyo tunayoiweza watanzania.Mpira ni burudani lakini kwa upande mwingine mpira ni vita tena ni vita kubwa sana sana.Sitaki kuongea mengi leo maana nitakuwa kama nimemeza kanda na maneno yanajirudia yaleyale.Kwa kifupi tuache maneno tuanze maandalizi sasa wakati ni huu na wala hatujachelewa.Asanteni sana na ni matumaini yangu kuwa sote kwa pamoja tutashikamana na kuanza maandalizi sasa.

Wednesday, November 28, 2007

CAMEROUN WANAFUNGIKA IWAPO TU...............

Wasomaji wangu wapendwa kwanza naomba niwaombe radhi kwa kutokuwepo hewani kwa takribani mwezi hivi hii yote inatokana na kuzidiwa na majukumu.Naomba radhi sana kwa hilo.Najua dada Salome wa Mtibwa Sukari,Deogratius Zegge wa Serena pale Tengeru Arusha na Mwandishi wa siku nyingi wa "gazeti la Daily Vision" la Kantalamba Sekondari pale Sumbawanga 1991-1993 bwana Boaz A. Boaz mtakuwa menisamehe baada ya kuwa sijaonekena kwa muda mrefu kidogo.
Leo nataka nizungumze juu ya kupangwa kwa ratiba ya kombe la dunia Afrika Kusini 2010 kule Afrika ya Kusini.Tupo kundi la kwanza katika kanda hii ya Afrika pamoja na vinara Cameroun,Visiwa vya Cape Verde na Mauritius.Kimahesabu kundi letu ni kama rahisi sana lakini kimchezo ni kundi la kati au wastani au kundi la kama watu wengine waonavyo la hizi timu tatu kuwa wasindikizaji wanaomsindikiza mfalme Indomintable Lions.
Mpira ni mchezo wa maandalizi,juhudi,maarifa kujitoa,kujituma na pia mchezo wa makosa.Cameroun wanajielewa kuwa wao ni wababe lakini kamwe hawawezi kjidanganya kuona kuwa timu kwazo walizopangiwa nazo ni vibonde.Tukumbuke kuwa hawakuwepo Ujerumani na wanalitambua hilo na wanajua machungu ya kukosa kushiriki fainali hizo kwa wao kukosa penati nyumbani.Hawatakubali kufungika na wanaweza kuwa na hasira sana hasa ukizingatia kuwa hwakuwepo katika fainali zilizopita kama kawaida yao.Hawawezi kukubali wazikose fainali hizi tena zinazochezwa katika bara hili la hapa nyumbani.Kwa kifupi Wana Wa Cameroun wanatambua kuwa kundi walilopangwa nalo kwa soka la siku hizi si timu vibonde hivyowako tayari kupigania nafasi yao kuliko vile watu wengine wafikiriavyo kuwa wamepangiwa timu vibonde!Wana EWa Cameroun wataingia kupigana na wanajua kuwa nguvu ya adui zao ni kubwa kutokana na soka la siku hizi kuwa limekuwa sana.Halikadharika hizi timu zingine pia zinajua kuwa yupo mfalme wa kundi nasi pia tujitahidi tuzifunge timu zingine!Kifupi kundi letu kila timu inapiga hesabu za kivyakevyake ili waweze kufanikiwa.
Ninachotaka kusema ni kuwa Cameroun wanafungika lakini wanafungika tu iwapo tutaanza maandalizi mapema tutaanza maandalizi sasa hivi tutaanzana maandalizi leo na wala siyo kesho!Cameroun atafungika tu iwapo tutaacha malumbano ya kuwa wachezaji gani ni bora na wachezaji gani siyo bora!Cameroun atafungika tu iwapo tutashikamana wote na pia tutampa mwalimu sapoti kubwa sisi sote kama watanzania na tunoitakia mema timu yetu.Maandalizi yaanze sasa kupata mafunzo nje ya nchi,kupata mechi za majaribio kutokukata tamaa sote lazima tushikamane kwa umoja wetu tutaiweza safari ya Afrika Kusini na Angola 2010 na hakika tunaweza kuishangaza dunia.Watanzania hakuna lisilowezekana katika sayari hii ni mipango madhubuti na mikakati ya maana tu ndiyo itakayoweza kutukomboa kutoka katika utumwa wa kuwa wasindikizaji."TUJIKWAMUE SISI WENYEWE KUTOKA KATIKA MAWAZO YA KUWA WASINDIKIZAJI HAKUNA ATAKAYETUFANYA KUWA HURU ILA NI SISI WENYEWE!"
Boaz,Salome na Deo nisaidieni kuwaeleza watanzania kuwa haya mambo yanawezekana iwapo tutakuwa na maandalizi ya maan akutoka sasa.Naomba mnisaidie kuwaeleza watanzania wote!Nisaidieni kwa njia mbalimbali kwa kupiga kelele kwa vipeperushi,kwa kuwajulisha watu mbalimbali na kwa kutumia njia zozote zile kwazo zinafaa kufikisha ujumbe kwa jamii ya watanzania.Kombe la dunia inawezekana!TWENDE TUJIANDIKISHE SASA WAKATI NI HUU!
Mwaka 2010:
Nchi:Afrika Kusini
Mji:J'burg
Uwanja:FNB Stadium
Kundi A:Mabingwa Italy,Spain,Japan,Tanzania
Mechi ya ufunguzi:Mabingwa Italy vs Tanzania
Matokeo ya mechi:Tanzania 1-Italy 1.
Tanzania leo imetoka sare na mabingwa wa dunia Italia kwa kufungana bao 1-1 katika mchezo uliochezwa katika uwanja wa First National Bank mjini J'burg katika mechi ya kwanza ya ufunguzi wa kombe la dunia hapa katika bara la Afrika.Ikumbukwe kuwa nchi hii ya Tanzania ndiyo mara yake ya kwanza kushiriki fainali hizi za kombe la dunia na pia ndiyo mabingwa wa kombe la Afrika kwa mwaka huu walilolitwaa mapema mwaka huu katika fainali za mataifa huru ya Afrika huko Angola baada ya kuwafunga mabingwa watetezi Misri huko mjini Luanda Angola.Mechi zijazo za Tanzania ni dhidi ya Japan na halafu itamalizia mechi zake kwa kupambana na Spain.
Hya mambo jamani yanawezekana ni suala la maandalizi tu na mipango madhubuti.Hakika inawezekana kama tumedhamiria na kama kweli tunataka kuwa washindani wa kweli.Asanteni sana na shime tuanze maandalizi sasa wakati ni huu bado hatujachelewa.