Mwanamuziki Bob Marley katika wimbo wake mmoja anaimba kuwa every where is a war,war in west,war in east,war up north,war down south,look every where is a war....
Sasa mtu unakaa unajiuliza kuwa kwa nini tunapigana?Kwa ajili ya nini?Je vita ni suluhisho la matatizo yote yanayomkabili mwanadamu?
Hivi kweli njia za amani zimeshindikana kutatua migogoro ya vita sehemu mbalimbali duniani?Tunapigana kwa ajili ya nini hasa.Watu wanachinjana kwa kutafuta kitu gani na je ni kweli Mwenyezi Mungu anapendezwa na mambo yote haya yanayotokea duniani?Kama jibu ni hapana kwa nini basi tunakubali kufarakana sisi wote binadamu humu ulimwenguni?Haya ni maswali amabayo sisi binadamu tunapaswa kujiuliza sana sana.Kuwa kwa nini tunapigana ni kwa ajili ya nini na je kwa nini kuwa katika hali tete kama hizi na je zitadumu kwa muda gani?HUU NI UBABE GANI NA LAZIMA TUJIULIZE HITIMISHO LAKE NI NINI?
Monday, August 02, 2004
MPIRA TANZANIA UMESHUKA.
Mpira wa miguu katika nchi yetu umeshuka sana na bila jitihada za dhati basi tutakuwa wasindikizaji siku zote.Ni lazima jitihada za dhati zichukuliwe ili tuweze kufika mahala walipofika wenzetu.Bila kuacha ubabaishaji basi hatutafanikiwa hata siku moja.Tutabaki kuwa wasindikizaji siku zote.
Subscribe to:
Posts (Atom)