KITUO CHA KARUME:
DALADALA:TABATA-SEGEREA:
MUDA:JIONI:
Wakazi wa Segerea wengi wetu lazima tupandie hapo Karume tukageuze na basi mpaka mnazi Mmoja mana usafiri wa Segerea ni taabu kwelikweli.Konda kasimama mlangoni tunaingia bila wasiwasi maana si twaenda kugeuza nalo,tunalipa mara mbili "Kongo Mnazi ikirudi Segerea!"Konda kamuona mwanafunzi hana makuu mwanafunzi yule mpole konda anamzuia mlangoni dogo anafanikiwa kuingia anakaambele kwa dereva mahala pasipo na kiti,nmi nipo mbele dereva "Mangi" anaanza kumfokea kwa nini unafanya vurugu mlangoni ukiumia nani atakulipa?Anamtukana dogo kakaa kimya tu kachoka na anaonyesha woga.Naingilia kwani kafanyaje?Anajibu hujamuona kafanya vurugu mlangoni namuuliza vurugu gani maana konda kamzuia sasa angeingiaje?Anajibu wewe unatetea ujinga wewe mpumbavu namjibu wewe ndo mpumbavu maana mtoto hajafanya vurugu unasema kafanya vurugu.Tunajibizana mpaka mnazi.Pale watu kibao sasa ndo wanafanya vurugu za kweli na wanaweza kuumia kwa kugombania basi namtazama dereva kwa chati halafu nacheka sana sana mpaka watu wananishangaa nafikiri jibu amelipata kwa nini ninacheka ni kuwa je wale watu wote wakiumia kwa kugombania basi atawalipa?Maana wamefanya vurugu n yule dogo pale Karume hakufanya vurugu kaambiwa kuwa anafanya vurugu akiumia nani atamlipa?
Wanafunzi wanapata taabu sana katika jiji hili hasa nyakati zza asubuhi na jioni,wanakatazwa hata kukaa hata kama basi halijajaa.Ugomvi wa kijana yule na koda na dereva kisa ni 50/= anayolipa ndiyo inamfanya asithaminiwe utu wake.Lakini si yeye anayepanga bei hiyo yeye anaathiriwa na mfumo tu jamani.
Na nimechunguza sana madereva na makonda vijana ndiyo wanawanyanyasa vijana wenzao wadogo zao.Lakini fanya utafiti utagundua kuwa makonda na madereva watu wazima wenye familia kamwe hawawanyanyasi wanafunzi na iwapo imeshindikana kuwachukua watawaeleza kistaarabu,binafsi nimewahi kumshuhudia konda wa makamo akiwakataa watu wazima na kuwachukua wanafunzi watoto wadogo nyakati za jioni ili wawahi nyumbani!Iinapaswa wengine waige mfano huo japo kwa kutoa lugha ya kistaarabu jamani.
Thursday, September 27, 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment