Friday, October 12, 2007

JAMANI CHONDECHONDE ETI SIMBA NA YANGA NGOMA ITAPIGWA USIKU UWANJA MPYA!

Nimeshtushwa sana na habari kuwa mechi ya watani wa jadi itapigwa uwanja mpya wa taifa siku ya tarehe 24 mwezi huu usiku.Kwa kweli nimeingiwa na wasiwasi mkubwa kuhusu hiyo mechi kupigwa katika uwanja ule mpya na wa kisasa zaidi,kwa nini ninakuwa na wasiwasi na hiyo mechi ni kuwa ninaaelewa vizuri mashabiki wa timu hizi mbili kwa uharibifu wao ulikithiri sasa kama hatuutaki huu uwanja basi ngoma hiyo na ipigwe hapo.Sijawahi kuona washabiki wasio wastaaarabu katika medani ya soka kama washabiki wa timu mbili hizi.Hapa ninazungumzuia wale mashabiki wahuni waliokubuhu na wala siyo wote.Hawa mashabiki wao kuingia na chupa za mikoja ni kitu cha kawaida sana kwao,pia uharibifu ni jadi yao mifano ipo kwa pale uwanja wa zamani wa taifa walivyokuwa wakifanya uharibifu pindi timu moja inaposhinda au kushindwa wao ni uharibifu tu.
Ule uwanja ni wa gharama kubwa sana na mashabiki wa simba yanga huwa kwa kweli hawadhibitiki kwa hiyo kama mechi hiyo itapigwa hapo basi juhudi za makusudi zianze sasa jinsi ya kuwadhibiti na pia ufanyike utaratibu kuwa hawa mashabiwasikae pamoja kwa maana kuwa watenganishwe kwani mpaka sasa ule uwanja haujafunguliwa rasmi na haieleweki kuwa mashabiki wa pande zote mbili kuwa pande zao za kukaa ni zipi maana ni tofauti pale tulipokuwa tunashangilia stars wote tulijichanganya na kuwa wa moja sasa je kwa hili serikali na TFF wanafikiria au wanalionaje?
Jitihada za dhati na za makusudi zisipochukuliwa ule uwanja utapata uharibifu mkubwa sana na tutakuja kushangaa kwa jinsi kama hawa mashabiki wasipochukuliwa tahadhari hivi sasa bado mapema.Inawezekana na tujipange sasa kudhibiti mashabiki wahuni wasituharibie uwanja bali timu zao zishindwe zenyewe maana dimba ni kama Emirate mwanawane!