Friday, December 26, 2008

WATANZANIA NA HALI NGUMU YA MAISHA.

Watanzania jamani kadri miaka inavyokwenda ndiyo hali ya maisha kwa sisi tulio wengi inavyozidi kuwa mbaya,huku vikundi vya watu wachache ao wakineemeka kupitia migongo ya walala hoi ambao ndiyo wengi katika taifa letu hili linalojulikana kama changa kiuchumi lakini lenye kila raslimali za kutufanya tusiwe na maisha ya kuigiza.Nchi ina utajiri wa kutisha lakini watu wake ni masikini wa kutupwa.Je nini kifanyike ili kuondokana na hali hii jamani sisi watanzania?
Hebu angalia jinsi baadhi ya watu walivyo wabinafsi,angalia jinsi wanavyojipendelea wao wenyewe huku wakisahau mamilioni ya watanzania wenzao wanavyoteseka kwa masahibu mbalimbali yanayowakumba kila kukicha.Magonjwa,njaa,kukosa matibabu,miundo mbinu mibovu elimu duni na vitu vingi vya jinsi hiyo.Watanzania jamani bado tunaweza kuifanya nchi yetu ikawa katika hali nzuri tu kama tutakuwa wamoja na kujituma huku bila ya kusahauliana na kutengana na kubaguana.Shime tuangalie wapi tulipokosea ili tujipange upya kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu na wananchi wake.Karne hii ni ya kila mtu kuwa katika maisha bora mambo ya kusema kuwa eti sisi bado ni maskini kwa kweli yamepitwa na wakati hivyo inatubidi tuwe wamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana kwa ajili ya watu wa taifa hili na nchi yote kwa ujumla.Asanteni.

Wednesday, December 24, 2008

TIMU YA TAIFA HAIWEZI KUWA BORA KAMA VILABU HAVITAKUWA BORA!

Watanzania kwa kiasi fulani tumepiga hatua katikakuelekea kwenye soka la kweli la ushindani na kutambulika kimataifa katika ulimwengu wa soka yenye akili.Tumeonyesha kuwa tunawezakutoka katika ule ujulikanao uigizwaji tu wa kikomedi katika soka na kuelekea katika hali halisi ya soka lenyewe.

Timu yetu ya Taifa kwa kiasi fulani angalau nasema kuwa angalau maana sisi ni mabingwa wa kuanzisha mikakati ya muda mrefu na mfupi lakini ambayo huwa hatuitimilizi.Kwa nini nasema hivyo ni kwa sababu ya kuja kuona kuwa kweli tumeanza na muelekeo na timu ipo vizuri kisoka lakini baadaye tena tunakuja kupote njia na kuanza kupiga hatua mia nyuma.

Mara nyingi sana tumekuwa na mipango ya maendeleo lakini inavurugika bila kutarajia.

Ninachotaka kukisema watanzania wenzangu leo ni kuwa ili timu yetu iwe nzuri basi ni vema wadau wote wa soka la Bongo wakajitolea kwa hali na mali ili kuhakikisha kuwa vilabu vinakuwa na msingi mzuri wa kisoka ili iwe chimbuko la kupata wachezaji wazuri wa timu ya taifa.Hapa lazima tuwe na mipango madhubuti ya soka katika vilabu vyetu kwa maana vilabu vyetu mpaka leo bado vinajiendesha katika enzi ya ujima kabisa kitu ambacho tunatakiwa tuondokane nacho kwa sasa.

Simba Yanga Mtibwa na vilabu vingine vyote wakati ni huu tumechelewa lakini tunaweza kufanya vizuri kama tutaamua kuwatunaanza na tunaweza.Tuanze sasa kuwa klabu na si mahala pagumzo na uswahili vilabuni huku tukijidanganya kuwa tunjua sana soka.Tuamketuwe na timu za vijana tuwe na mipango kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu katika nyanja hii muhimu kabisa ya soka.Soka ni kazi kama kazi nyingine na si mahalapawatu waliokosa kazi kuwa sehemu ya kupakimbilia jamani.Soka ni ajira kama zilivyo ajira zingine soka ni kazi soka ni vita sokani mipango ya kweli na uhakika na si kuwa na mipango ya kikomedi. Soka Watanzania wenzangu ni kujitoa kwa halina mali.Hatujachelewa na tuanzse sasa.Asanteni.