Thursday, November 29, 2007

WATANZANIA KUNDI LETU NDILO GUMU WALA SI RAHISI!

Kuna baadhi ya watu wameanza kuwadanganya watanzania nasi watanzania ni wepesi wa kuamini mambo ambayo kwa hakika huwa si ya kweli kabisa!Kumbuka jinsi watu walivyokuwa na matumaini ya kwenda Ghana kila mmoja alijua kuwa mwakani sote macho yetu kideoni tukiwashangilia Stars na Stars nao masikini wakaanza kuvimba vichwa wakati hata safari bado ilikuwa mbichi kabisa!Kumbuka jinsi walivyokuwa na nyodo wakati wanakwenda kucheza na Zambia kule mji unaotamani angalau kuwa na bahari japo kwa siku moja,Morogoro,washabiki waluguru wale wamefika Msamvu kuwalaki wachezaji wao lakini Stars wakawafungia vioo maana tayari wao wameishakuwa wafalme!
Ninachotaka kusema siyo kukatisha tamaa la hasha bali kuwaasa watanzania wenzangu kuwa kundi letu si rahi ni gumu sana na pengine ndilo kundi gumu kuliko makundi yote katika safari hii ya kuwania tiketi ya kucheza kombe la dunia.
Tukumbuke kuwa kwa soka la kisasa hakuna kitu kinachoitwa timu rahisi au kundi rahisi kama nilivyosema jana kuwa mpira ni mchezo wa maandalizi kama mitihani,mpira ni mchezo wa kujitoa,kujituma,kupambana na si kucheza soka ya midomoniambayo ndiyo tunayoiweza watanzania.Mpira ni burudani lakini kwa upande mwingine mpira ni vita tena ni vita kubwa sana sana.Sitaki kuongea mengi leo maana nitakuwa kama nimemeza kanda na maneno yanajirudia yaleyale.Kwa kifupi tuache maneno tuanze maandalizi sasa wakati ni huu na wala hatujachelewa.Asanteni sana na ni matumaini yangu kuwa sote kwa pamoja tutashikamana na kuanza maandalizi sasa.

1 comment:

Anonymous said...

thanks for visiting my blog!!! yes, thanks to my sister i was able to understand yesterday!! wish she was here to translate today :-)