Friday, December 26, 2008

WATANZANIA NA HALI NGUMU YA MAISHA.

Watanzania jamani kadri miaka inavyokwenda ndiyo hali ya maisha kwa sisi tulio wengi inavyozidi kuwa mbaya,huku vikundi vya watu wachache ao wakineemeka kupitia migongo ya walala hoi ambao ndiyo wengi katika taifa letu hili linalojulikana kama changa kiuchumi lakini lenye kila raslimali za kutufanya tusiwe na maisha ya kuigiza.Nchi ina utajiri wa kutisha lakini watu wake ni masikini wa kutupwa.Je nini kifanyike ili kuondokana na hali hii jamani sisi watanzania?
Hebu angalia jinsi baadhi ya watu walivyo wabinafsi,angalia jinsi wanavyojipendelea wao wenyewe huku wakisahau mamilioni ya watanzania wenzao wanavyoteseka kwa masahibu mbalimbali yanayowakumba kila kukicha.Magonjwa,njaa,kukosa matibabu,miundo mbinu mibovu elimu duni na vitu vingi vya jinsi hiyo.Watanzania jamani bado tunaweza kuifanya nchi yetu ikawa katika hali nzuri tu kama tutakuwa wamoja na kujituma huku bila ya kusahauliana na kutengana na kubaguana.Shime tuangalie wapi tulipokosea ili tujipange upya kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu na wananchi wake.Karne hii ni ya kila mtu kuwa katika maisha bora mambo ya kusema kuwa eti sisi bado ni maskini kwa kweli yamepitwa na wakati hivyo inatubidi tuwe wamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana kwa ajili ya watu wa taifa hili na nchi yote kwa ujumla.Asanteni.

No comments: