Unajua sijui nijiite mzembe au msahaulifu hata sijui nisemeje,kwa kweli nilisahau namba yangu ya kificho hata nashindwa sijui nisemeje,eti nimehangaika sana leo ndiyo nimebahatika kuipata.Kwa kifupi hii blog yangu niliifungua toka February 2004 hebu fikiria miaka karibu mitatu lakini nikawa nashindwa hata kuandika kitu cha kuipa jamii kwa kujifanya niko bize sijui bize gani?Bize nitakuwa mimi bwana bize wako kina Ndesanjo maana wao kila kukicha wanahangaika kila mahala kutuhabarisha na kutuelimisha.
Lakini baada ya kusoma tena na tena makala ya Ndesanjo yatokayo katika gazeti la Mwananchi kuwa kila mtu ni mwana habari haijalishi kuwa kasomea au la lakini pale alipo na akiona habari yoyote basi ni habari basi nikashawishika kuwa anagalau niwe ninajitahidi kuwapatia wanajamii habari mbalimbali zitukiazo katika maisha yetu ya kila siku.
Bwana Boaz A. Boaz Mwandishi wa zamani wa gazeti la shule Kantalamba 1991-1993 "Daily Vision" nashukuru kwa komenti yako na kuni unga mkono hasa kutokana na matokeo ya Taifa Stars na The Mambaz pia nilijaribu kumuuliza mchezaji mahili wa zamani wa Tanzania Sekilojo Jonson Mbwambo Chambua a.k.a. baba Lisa naye akasema kuwa matokeo yale aliyatarajia kwa maana kuwa wachezaji wa sasa wanapewa kila kitu lakini hawana mbinu afya maarifa nguvy na ari ya kutetea taifa lao.
Cha msingi kama nilivyoseni kuwa inabidi tugeuke nyuma kuangalia soka la watoto na vijana na kupata waalimu bora na wenye mbinu ya kuwafundisha hao vijana na ikiwezekana zianzishwe shule maalumu za soka kama kweli tunataka tufanikiwe na kamwe tusitake mafanikio ya njia za mkato hayo kamwe katika soka hayapo.Tutafanikiwa kama tutaanza sasa wala hatujachelewa!Asante
Monday, September 24, 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment