Hakuna aliyetarajia kuwa Wakongwe wa soka hapa nchini?Au wavurugaji wa soka hapa nchini?Kuwa wataangukia pua mwishoni mwa wiki iliyopita katika safari ndefu ya kusaka bingwa wa Tanzania bara wa soka msimu wa 2008/2009.Simba na Yanga wameonja makali ya kufungwa katika mechi zao za mwanzo kabisa msimu huu.Binafsi nimefarijika sana na vipigo hivyo kwa hawa wavurugaji wa soka la hapa Bongo.Hii ni changamoto kwa viongozi na wapenzi wa timu kubwa hizi mbili ambao wamejikita katika mawazo ya kuwa wao ndo kila kitu katika soka la Bongo na kuwa bila wao hakuna kitu kiitwacho soka kinaweza kufanyika hapa Bongo.
Wadau wa timu kubwa hizi mbili kwa kweli wanashindwa kusoma alama za nyakati kuwa kwa zama hizi ni kuwa soka linapita katika mabadiliko makubwa sana hasa baada ya kuwa timu yetu ya Taifa imeboreshwa kwa kiwango cha kuridhisha na kuwa kamwe wasitegemee timu kama Ashanti kuwa zama hizi inaweza kucheza bila ya malengo kamwe kamwe maana kila ndoto ya mchezaji wa nchi hii katika timu hizi ni kuwa na mafanikio makubwa katika soka hili la kisasa ambalo kwao linalipa siku hizi.
Wachezaji wa timu hizi ndogo siyo kuwa hawana akili wanajua kuwa hizi ndiyo nafasi zao adimu na pekee kwa wao kuonekana ili kuchaguliwa timu ya taifa na hatimaye kuweza kuonekana na kupata timu nje ya nchi ili kukuza vipaji vyao na kuendelea kimaisha.
Binafsi ni mnazi mkubwa wa Simba lakini napenda kusema hadharani kuwa ushabiki wangu ni tofauti kidogo na wanazi wengine wa timu kubwa hizi.Mimi naishabikia Simba iwapo inaonyesha kiwango kizuri,na haibebwi na marefa au watu fulanifulani wenye marengo yao binafsi. Lakini kama naona kuwA ushindi wake una mizengwe na ni wakutiliwa mashaka kamwe huwa siwi upande wao!Pia kama timu ya Yanga inacheza vizuri mechi za nje yaani za kimataifa basi huwa ni mmoja wa mashabiki wanaojumuika na wanayanga kuipa sapoti ya kuishangilia.
Huwa napenda sana timu kubwa hizi zinapokutana zenyewe au zichezapo na timu pinzani basi zishinde kwa uwezo wa timu na si kwa uwezo wa watu fulani wachache,hapa ndiyo maana nafika mahala nasema kuwa timu hizi ni wavurugaji wakubwa wa soka la bongo.
Lazima Simba na Yanga watambue kuwa Kukua kwa viwango vya mpira katika timu hizi si kwa mmoja kumfunga mwenzie bali ni kuwa na mikakati madhubuti ya kuhakikisha kuwa zinakuwa moja ya vilabu vikubwa kabisa katika ukanda wa soka wa Afrika na wakidhamiria wanaweza.
Wasipende kuwa na wachezaji wa magazetini au kuwa na wachezaji wa kusifiwa na wapenzi wao mara baada ya usajili na kuonekana mazoezini na kusifiwa kuwa safari hii timu yetu kiboko makombe yote yatakuwa yetu huu mwaka wa vikombe Msimbazi,huu mwaka wa vikombe Jangwani na vitu kama hivyo.Mpira siyo mdomoni mpira ni uwanjani na maandalizi ya muda mrefu na yenye marengo.Mpira tofauti na msanii wa Runinga kuwa anaweza akatunga kitu hapohapo na akapata mashabiki.Simba na Yanga imefika wakati sasa waelewe kuwa mpira siyo "Masanja Mkandamizaji",mpira siyo "Uswahili" mpira kazi kama kazi zingine.
Naelewa kuwa kufungwa huku na kutoka sare kutawafanya waanze kutafuta mbinu za ziada ndani na nje ya uwanja nasema hizo hazitawasidia maana watanzania sasa wamekuwa waelewa kwani watazigundua mbinu hizo hata kama watakuwa wanashinda kwa msaada wa watu fulanifylani lakini lazima watambue kuw mbinu hizo hazitawafikisha popote cha muhimu ni kuucheza mpira na kuacha usanii.Waache timu bora zishinde na wala siyo bora timu ishinde.
Ashanti,Coastal Union nawapongeza sana kwa kuvikandamiza vigogo mmenikumbusha enz ya Relinya Morogoro.Cha msingi msibweteke safari bado ni ndefu na hizi timu zina mbinu nyingi sana ya kuweza kukudhoofisheni.SIMAMENI IMARA PIGANIENI HAKI ZENU KWA KUCHEZA MPIRA NA KUWA MAKINI MUDA WOTE WA MCHEZO!KUMBUKENI KUWA SIMBA NA YANGA ZINA MBINU NYINGI SANA.MSIBWETEKE.MSIJE MKAWA KAMA WAPIGANAJI WA OMAR TUPAC SHAKUR MILITIA MOVEMENT WALIPOTEKA UBALOZI WA JAPAN KULE LIMA,PERU 1997 WAKAJISAHAU NA ULINZI WAKAANZA KUCHEZA SOKA KAZINI,UNAJUA KILICHOWAKUMBA?MAKOMANDOO WAKAWAVAMIA PASI NA HABARI NDO IKAWA IMETOKA HIYO!SIMBA NA YANGA NI MAKOMANDOO NA MAFIA WA SOKA LA KIBONGO MSILALE LETENI MAPINDUZI YA KWELI HATA WAKIPENDELEWA WATU WATAONA!ASHANTI,COASTAL NA TIMU ZOTE CHANGA ALUTA CONTINUA!JIKWASMUENI NINYI WENYEWE KUTOKA KATIKA MAKUCHA YA SIMBA NA YANGA NA HAKUNA MTU ATAKAYEWABEBA BALI NI NI NINYI WENYEWE!SIMAMENI IMARA HAKI ZENU ZITAPATIKANA KWA SOKA LENU LA KUVUTIA,WAKATI WA SOKA LA VURGU KWENU ULISHAPITWA NA WAKATI ONESHENI MNAWEZA WATU KIBAO WAPO NYUMA YENU!USHINDI NI DHAHIRI!ASANTENI.
Thursday, September 27, 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment