Friday, February 06, 2009

JE TUMEMUELEWA MAMA ANNA TIBAIJUKA?

Kwa waliongalia kipindi cha TV cha Chanel Ten kinachojulikana kama "Je Tutafika kinachoendeshwa na mzee wetu Makwaia Wa Kuhenga akimhoji mama Tibaijuka kuhusu mauaji ya Maalbino nchini mwetu,sijui kama Watanzania wenzangu tulimuelewa vizuri yule mama wa Kitanzania msomi aliyebobea na mwenye kuheshimika sana Kimataifa.Napenda kumpongeza mama kwa jinsi alivyoweza kuisaidia jamii ya Watanzania kupitia kipindi kile ni kwa namna gani tutaweza kuzuia mauaji ya ndugu zetu Maalbino wasio na hatia.

Ameongea mambo ambayo hakuna hata mmoja wetu kuwa aliwahi kuwaza hata siku moja kuwa je ni njia gani tuweze kutafuta ilituweze kuzuia mauaji hayo?

Sina ya kuongea mengi lakini kama Chanel Ten wataweza kukirudia kile kipindi mara kwa mara ili Watawala wetu na Watanzania kwa ujumla tuweze kupata somo alilotoa yule mama wa Muleba ambaye anaishi na kuutumikia ulimwengu huu huko New York.

Mama Hongera sana kwa kweli umenikuna sana na nilikuelewa sana sana.Hakika tunatakiwa tuache kabisa kile ulichokiita kuwa "Stroke Brush Conclutions" kama sijakosea.Na pia kuwa kama ulivyosema kuwa lazima mtu anaposema kuwa amefanya utafiti basi uwe utafiti na si vinginevyo!

Mama somo lile ni la maana sana.Wasiwasi wangu je tumelielewa?Tujitahidi kwa bidii na maarifa tulielewe somo lile!Mzee Makwaia hongera kwa mumleta mama Anna kututatulia ili tupate ufumbuzi wa kuwakomesha hawa washenzi wasiostaraabika kwa kufikiri mawazo ya kipumbavu kuwa utajiri utatokana na viungo vya binadamu wenzetu Maalbino.Narudia tena kama tutayafuata yale aliyosema huyu mama basi tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa kukomesha kabisa mauaji ya ndugu zetu hawa jamani.Tukumbuke kuwa thamaniya binadamu haiwezi kufananishwa na kitu chochote kile.Asante.

No comments: