Wengi walikuwa na matumaini makubwa sana kuliko uwezo wa timu yetu ya Taifa baada ya mchezo wa kule Burkina Faso na kabla ya mchezo na ndugu zetu wa damu Msumbiji.Wachache sana tulitegemea au kutarajia kuwa lolote linaweza kutokea katika mechi ile maana nao Msumbiji wana uzoefu na pia walikuwa wnajiandaa.
Katika mchezo wa mpira kuna vitu vingi sana hata bahati pia ipo.Inawezekana kabisa kuwa tulikuwa na bahati BurkinaFaso na inawezekana pia Msumbiji walikuwa na bahati hapa kwetu.Lakini kusema ule ukweli ni kuwa siku ya mechi na Msumbiji wale jamaa walituzidi sana na hii inawezekana ilichangiwa siyo tu kujiamini kwa wachezaji wetu bali pia hata sisi washngaliaji na tukasahau majukumu yetu ya kumuua Mamba.
Hatimaye baada ya mchezo timu bora ikashinda hilo halina ubishi.Lkini je tumejifunza nini wtanzania?
Tusiwe watu wa kukata tamaa mapema kiasi hicho!Timu yetu ndiyo kwanza inajengwa tutakuja kuyaona tu mafanikio na kamwe tusipende mafanikio ya mkato.Ipo siku penye nia pana njia tushikamane tuwe pamoja tuwe wamoja kwa kushirikiana tutakuja kuyaona matunda baadaye na iyo sasa wakati ni huu shime shime!Ushindi waja!
Tuesday, September 18, 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Kwanza, hongera kwa kuanzisha blog yako. Kuna jambo moja kuhusu T/stars ambalo watanzania kama kawaida yao ya unafiki hawataki kulisema. Pamoja na sababu zingine zote zinazotolewa tatizo lingine ni kocha mkuu wa taifa stars. Lazima tukubali kuwa naye ni tatizo kubwa. Kwanini? yeye mwenyewe kasema alijua T/stars haiwezi kwenda Ghana, kwahiyo alishashindwa kabla. Swali kwanini hakutuambia wenye timu kuwa kwa mwenendo anaouna timu yetu haifai. Tungeweza kujua tufanyaje, sasa timu imetolewa ndio anasema, je tungeshinda angetoa maenoneo hayo. Kwa hilo tu ameonyesha kuwa ni mtu anayebahatisha tu. Hilo unaweza kuliona pia jinsi anavyopanga timu yake, unategeme mchezaji ambaye hajafunga zaidi ya mechi 15 za kimataifa na numbani ndio afunge goli kwenye crucial mechi kama ya mambas. Halafu toka kaanza kufundisha ni mchezaji gani ambaye tunaona hata kiwango chake binafsi kimeongezeka hakuna kabisa, viwango ni vile vile. Ukiongea na wachezaji wa stars watakwambia kwanini timu ilitolewa sababu wanaijua vizuri, ila waandishi wetu wa habari wa kibongo hakuna hata aliyefanya mahojiano nayo ya kiana kuhusu hilo
Post a Comment