Tuesday, September 25, 2007

SOPA LODGE,NGORONGORO KRETA! 2005-2006:

Sehemu ya kuvutia mojawapo ya yanayosemwa maajabu ya dunia.Kwa mara ya kwanza katika maisha yangu ninaiona kretakwa mbali toka katika hii hoteli ya Sopa Lodge amabayo tumekuja kufanya majaribio kwa vitendo kwa muda wa miezi mitatu.
Watu wakarimu hapa na tumepokelewa vizuri sana jamaa kaja mpaka ndani ya gari kuja kutupokea na kutuonyesha wapi tutapumzika kwa usiku huo tuliofika.Baridi ni kali sana tumepewa blanketi mbilimbili lakini bado tunasikia baridi.
Kesho yake tunaonyeshwa kwa uongozi wa hoteli na kupangiwa majukumu ya kujifunza kwa muda huo wa miezi mitatu,kutoka Disemba mpaka Machi mwaka ujao.
Tunachapa kazi wanachuo tuliotoka mjini Arusha katika chuo cha mafunzo ya hoteli.Tunaanza kuzoeana na wafanyakazi,dada mmoja mweupe kwelikweli anatuzoea na kutupa majina ya utani "wanafunzi wangu".Dada huyu ananizoea sana mimi kuliko mwenzangu Tom aasema mimi mcheshi na ninatoka Dar na yeye anasifia Dar anadai huwa anakuja mara nyingi kwa jamaa yake.Baada ya siku kadhaa Mkuu wangu wa jiko hataki kuona huyu dada ananizoea anaanza kuwa makali kwangu na kufoka bila sababu baada ya kuchunguza kumbe ati alimfundisha mambo mengi ya upishi na inadaiwa ni bibi yake sasa Mpishi anawasiwasi naweza fanya mapinduzi baridi!Anakuwa mbogo ile mbaya.Naona naonewa naamua kuwaka siku moja usiku ile mbaya mpaka walinzi wa hoteli wanashangaa huyu Trainee haogopi anamwakia jamaa ile mbaya.Rafiki yangu Ray ananifuata asubuhi anasema safi sana usingeonyesha msimamo angekunyanyasa sasa atakuwa anakuogopa!
Huko ni hotelini.Njoo sasa kambini mahala tulalapo,madereva wa Tours wnanishangaa jamaa anamuuliza mwenyeji eti masai huyu jamaa naye ni Trainee?anaambiwa ndiyo anasema hapana sasa tunadanganyana sasa tumeanza kuletewa wapelelezi kambini!Unajua kisa cha jamaa kusema hivi?Kiumri kwa sisis tuliokuja kujifunza mimi ni mkubwa pamoja na mwenzangu Tom lakini waliobakia wote ni vijana waliomaliza shule ya sekondari mwaka jana au juzi sasa mimi jamaa wanashangaa nina kipara kikubwa sana hata mwanzoni askari mmoja wa TANAPA alifikiri nanyoa kama mtindo!Njaribu kuwaeleza kuwa ukubwa wa umri si kikwazo katika kusaka ujuzi.
Napata marafiki wengi sana wa Kimasai na watu wa sehemu mbalimbali wengine wananiita Babu,wengine wananiita Mourinhonmaana kwa mpira ndiyo usiseme naupenda na nimekuwa nikiwapa data hata za miaka ya nyuma sana.
Kombe la Mataifa ya Afrika linaanzaMisri Januari hiyo bado tupo mafunzoni napangiwa shift mbaya sana wakati musada wa mechi inaanza.Nampiga kamba kiongozi wangu inabidi nidanganye kuwa huwa napata "majani" kidogo sasa naomba nikapate ingawaje sijawahi kupata majani hata siku moja jamaa anasema wewe nenda usichelewe kurudi nakimbia kambini nacheki kama dakika 30 narudi tena.
Maisha yanenda napata marafiki wengi na kujifunza kazi nyingis sana.Lakini katika yote niliyoyaona Ngorongoro Nilishangazwa na kupendezwa sana na Kreta.Nilipofika chini kabisa kule kwa mara ya kwanza nilichanganyikiwa sikuyaamini macho yangu.Dr.Remi aliwahi kuimba kuwa tembea ujionee usingoje kuambiwa huwezi ukafananisha Morogoro na Dar es salaam ni kweli Ngorongoror ni mojawapo ya maajabu ya dunia!Kwa kweli kunapendeza sana!

No comments: